MABINGWA watetezi, Simba SC wanatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kesho asubuhi kwa ndege kwenda Mwanza Alhamisi watacheza mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kufuatia wenyeji, Ruvu Shooting kuamua hivyo, tofauti na kawaida yao mechi zao dhidi ya Simba na Yanga kuchezea Dar es Salaam badala ya Mlandizi mkoani Pwani, ambao Uwanja wao wa Mabatini haukidhi vigezo vya mechi za mashabiki wengi.




from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/34v1mdU
via gqrds