MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina, Sergio Aguero ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Barcelona kufuatia kusaini mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru kufuatia kuondoka Manchester City.
Nyota huyo anayefikisha umri wa miaka 33 kesho, aliichezea kwa mara ya mwisho Man City Jumamos iliyopita katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikichapwa 1-0 na Chelsea nchini Ureno.
Aguero alijiunga na Man City akitokea Atletico Madrid mwaka 2011 na kuifungia klabu hiyo mabao 260 akiiwezesha kushinda mataji matano ya Ligi Kuu England, moja la FA Cup na sita ya Kombe la Ligi.


Kisoka Aguero, aliibukia Independiente ya kwao, Argentina kabla ya kuhamia Atletico mwaka 2006, ambako alifanikiwa kushinda taji la where he won the Europa League mwaka 2010.


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/3yU78DB
via gqrds