KLABU ya Azam FC imeingia mkataba mpya wa miaka miwili zaidi na mshambuliaji wake wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo, ambao utamfanya awe mali wa klabu huyo hadi mwaka 2024.
"Dube ambaye tumemsajili msimu huu, amekuwa na kiwango bora kabisa hadi sasa akiwa ndiye kinara wa ufungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) akiwa na mabao 14," amesema Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
Mbali na mabao hayo 14, kwa ujumla msimu huu, Dube amefunga mabao 17 kwenye mashindano yote, mengine matatu akitupia katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).




from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/3g6X2Xu
via gqrds